Laini ya Moja kwa Moja ya Uzingatiaji ya Universal

Kwa kupiga simu bila malipo:

Kupiga simu nje ya nchi wasiliana na opareta wa nchini mwako. Omba kupiga simu ambayo mpokeaji atailipia (reverse call) kwa kupiga namba ya marekani, ambayo imeorodheshwa hapa chini:

503-748-0657

Opareta akiuliza ni nani anayepiga simu, taja jina la kampuni yako. Usitaje jina lako. Simu zote za kumtoza gharama mpokeaji (Reverse Call Charges), zitakubaliwa na Kituo cha Masiliano cha EthicsPoint.

Wavuti: www.ethicspoint.com

Kupiga simu moja kwa moja kwa masaa 24, siku 7 za juma.

Mtu yoyote anayetoa taarifa kupitia simu ya moja kwa moja ya Uhakiki hahitajiki kutoa jina lake au taarifa yoyote ya kumtambulisha, na hakuna kitambulisho cha mpiga simu au kutumika kwa vifaa vya kurekodia.

Wasiliana Nasi:

Harvard Smith
Ofisa Mkuu wa Utekelezaji
Universal Corporation
9201 Forest Hill Avenue
Stony Point II Building
Richmond, Virginia 23235
(mstari wa moja kwa moja) +1 804 254 1316
(ofisi) +1 804 359 9311
(faksi) +1 804 254 3594
(email) compliance@universalleaf.com

Barua ya Mwenyekiti

Wapenzi wafanyikazi wenzangu:

Familia ya makampuni ya Universal Corporation imekuwa ikifanya biashara kwa kujivunia kwa zaidi ya miaka 100. Wakati huo, watu wetu duniani kote wamejitahidi kujenga raslimali yetu muhimu zaidi ya biashara — Uadilifu.

Tukiangalia mbele, tunafaa kudumisha raslimali hii ya thamani. Kutekeleza biashara yetu kwa uadilifu ni muhimu kudumisha hadhi yetu kama kiongozi wa sekta yetu. Tunawajibika kwa wateja wetu, jumuiya zetu, washikadau wetu, na kila mmoja wetu. Sote tuko na jukumu la kutekeleza, na Universal inakutegemea.

Kanuni zetu za Maadili huweka viwango vya juu vya kimaadili kutuongoza. Kufanya biashara kulingana na viwango vya juu vya kimaadili ndio kitu cha sawa kufanya, na pia ni biashara nzuri. Ikija kwa maadili na uadilifu, hapa Universal tuko na malengo matatu ya mwanzo: 1) fanya kazi kwa uadilifu; 2) fanya biashara kwa uadilifu na 3) shughulikia taarifa na raslimali kwa uadilifu. Tunapofikia malengo hayo, tunaifanya Universal kuwa kampuni inayostahili kuwa.


Wako mwaminifu,George C. Freeman III
Mwenyekiti, Rais, na Afisa Mkuu Mtendaji

Rasilimali za Uzingatiaji